Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 usajili Tume chini ya Sehemu hii anaweza kuwasilisha rufaa kwa njia ya maandishi kwa Waziri. Usajili wa taasisi za umma 21. Mara baada ya kuanza kutumika kwa Sheria hii, taasisi za umma zinazoshughulika na ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi zitachukuliwa kuwa zimesajiliwa chini ya Sheria hii na zitapaswa kuzingatia masharti ya Sheria. SEHEMU YA NNE UKUSANYAJI, UTUMIAJI, UFICHUAJI NA UHIFADHI WA TAARIFA BINAFSI Ukusanyaji wa taarifa binafsi 22.-(1) Sehemu hii itatumika kwa(a) ukusanyaji na uchakataji wowote wa taarifa binafsi uliofanywa kwa taarifa yote au sehemu ya taarifa hiyo kwa njia ya kielektroniki au isiyo ya kielektroniki; (b) uchakataji wa taarifa binafsi unaofanywa katika utekelezaji wa majukumu ya mkusanyaji anayeishi katika Jamhuri ya Muungano au katika sehemu ambayo sheria za Jamhuri ya Muungano zinatumika kwa mujibu wa sheria za kimataifa; (c) uchakataji wa taarifa binafsi unaofanywa na mkusanyaji au mchakataji anayeishi nje ya Jamhuri ya Muungano, ikiwa uchakataji huo umefanyika nchini na sio kwa madhumuni ya kupitisha nchini taarifa binafsi kwenda nchi nyingine. (2) Mkusanyaji atakusanya taarifa binafsi iwapo(a) taarifa binafsi inakusanywa kwa madhumuni halali yanayohusiana na kazi ya mkusanyaji; na (b) ukusanyaji wa taarifa binafsi ni muhimu au unatokana, au kuhusiana moja kwa moja, na madhumuni halali. (3) Mkusanyaji hatakusanya taarifa binafsi kwa njia zisizo halali. Chanzo na utoaji wa taarifa binafsi 23.-(1) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (3), mkusanyaji atakusanya taarifa binafsi moja kwa moja kutoka kwa mhusika wa taarifa. (2) Kabla ya kukusanya taarifa binafsi, mkusanyaji atahakikisha kuwa mhusika13

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents