Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
(g) namna ambayo Tume ilifahamu kuhusu
ukiukwaji, ikijumuisha endapo mkusanyaji au
mchakataji aliifahamisha Tume;
(h) kiwango ambacho mkusanyaji au mchakataji
alizingatia notisi za utekelezaji na notisi za
adhabu zilizowahi kutolewa awali;
(i) uzingatiaji wa kanuni za maadili au vigezo na
masharti ya usajili;
(j) endapo adhabu itakuwa na ufanisi; na
(k) kigezo kingine chochote kinachoweza kutumika
kuongeza au kupunguza adhabu, ikiwa ni
pamoja na faida za kifedha alizozipata au
hasara alizosababisha, moja kwa moja au
vinginevyo, kutokana na ukiukwaji huo.
Faini za
kiutawala
47. Kiwango cha juu cha adhabu kinachoweza
kutolewa na Tume katika notisi ya adhabu kuhusiana na
ukiukwaji wa masharti ya Sheria hii, ni shilingi milioni
mia moja.
Marejeo ya
uamuzi
48.-(1) Tume baada ya kuombwa au kwa utashi wake
yenyewe inaweza kufanya marejeo ya uamuzi na
maelekezo yake iliyoyatoa kwa mujibu wa masharti ya
Sehemu hii.
(2) Baada ya kufanya marejeo kwa mujibu wa
kifungu kidogo cha (1) Tume inaweza kutengua,
kubadilisha au kusitisha uamuzi au maelekezo yake
iliyoyatoa awali.
Haki ya rufaa
49. Mtu ambaye hataridhika na hatua yoyote ya
kiutawala itakayochukuliwa na Tume, ikiwa ni pamoja na
maelekezo yaliyotolewa katika notisi ya utekelezaji au
adhabu iliyotolewa katika notisi ya adhabu, anaweza
kukata rufaa Mahakama Kuu.
Malipo ya fidia
50.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 37,
Tume inaweza pamoja na adhabu nyingine zilizotolewa
chini ya Sheria hii, kumuamuru mkusanyaji au mchakataji
aliyesababisha madhara kwa mhusika wa taarifa kutokana
na ukiukwaji wa masharti ya Sheria hii kulipa fidia kwa
mhusika wa taarifa.
27
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents