Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
Makadirio ya
mapato na
matumizi na
udhibiti wa
fedha
53.-(1) Mkurugenzi Mkuu atapaswa, katika kipindi
kisichopungua miezi mitatu kabla ya mwisho wa kila
mwaka wa fedha, kuandaa na kuwasilisha katika Bodi ili
kuidhinisha, bajeti inayojumuisha makadirio ya mapato na
matumizi kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha.
(2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha
(1), Tume itawasilisha nakala ya bajeti kwa Waziri kwa
ajili ya kuidhinishwa.
(3) Waziri anaweza kuitaka Tume kufanya
marekebisho katika bajeti ikiwa kwa maoni yake bajeti
haiwakilishi makadirio sahihi na ya kuridhisha ya mapato
na matumizi.
Matumizi ya
fedha
54. Matumizi hayatafanyika kutoka kwenye fedha za
Tume isipokuwa kama matumizi hayo ni sehemu ya
matumizi yaliyoidhinishwa na Bodi chini ya kifungu cha
53(1) kuhusiana na mwaka wa fedha ambao matumizi
yaliidhinishwa.
Makadirio ya
nyongeza
55.-(1) Bodi inaweza, wakati wowote kabla ya mwisho
wa mwaka wa fedha husika, kuandaa na kuwasilisha kwa
Waziri kwa ajili ya kuidhinishwa makadirio yoyote ya
nyongeza ya makadirio ya mwaka husika.
(2) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1),
Mkurugenzi Mkuu anaweza, pale ambapo dharura
imetokea katika utekelezaji wa majukumu ya Tume,
kufanya matumizi ambayo hayajaidhinishwa na Bodi
ambapo Mkurugenzi Mkuu atalazimika, ndani ya miezi
mitatu inayofuata, kuomba idhini ya Bodi kwa matumizi
hayo.
Akaunti na
ukaguzi
56.-(1) Tume itaweka vitabu vya hesabu na kutunza
kumbukumbu sahihi za shughuli zake kwa mujibu wa
viwango vya uhasibu.
(2) Tume itapaswa, ndani ya miezi sita baada ya
mwisho wa kila mwaka wa fedha, kuandaa ripoti ya
utekelezaji wa majukumu yake katika mwaka huo wa
fedha, na nakala moja ya ripoti hiyo pamoja na nakala ya
hesabu zilizokaguliwa zitawasilishwa na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
29
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents