Na 11 Sura ya 286 Taarifa za kila mwaka na mikataba ya utekelezaji Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (3) Hesabu za Tume zitakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali au mtu mwingine aliyesajiliwa kama mkaguzi chini ya Sheria ya Usajili wa Wakaguzi na Wahasibu aliyeteuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa dhumuni hilo. 57.-(1) Ndani ya muda wa miezi miwili baada ya kupokea hesabu zilizokaguliwa na taarifa ya mkaguzi wa hesabu, Mkurugenzi Mkuu atapaswa kuwasilisha kwa Waziri taarifa ya mwaka husika ikijumuisha(a) nakala ya hesabu zilizokaguliwa pamoja na taarifa ya mkaguzi kwenye akaunti hizo; (b) taarifa ya utekelezaji wa malengo muhimu na taarifa nyingine yoyote inayohusiana na utekelezaji wa malengo hayo; (c) taarifa ya uendeshaji wa Tume katika mwaka wa fedha husika; na (d) taarifa nyingine kama ambavyo Waziri anaweza kuhitaji. (2) Waziri atawasilisha Bungeni nakala ya taarifa ya mwaka ya Tume ndani ya miezi miwili au katika mkutano wa Bunge unaofuata. SEHEMU YA TISA MASHARTI MENGINEYO Mazingira yanayoondolew a katika mawanda ya Sheria hii 58.-(1) Hakuna chochote katika kifungu hiki kitakachomuondolea mkusanyaji au mchakataji wajibu wa kuzingatia misingi ya sheria katika ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi na uchukuaji wa hatua muhimu katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa taarifa binafsi alizonazo. (2) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1), uchakataji wa taarifa binafsi unaweza kuondolewa katika mawanda ya masharti ya Sheria hii ikiwa uchakataji huo(a) unafanywa na mhusika wa taarifa katika shughuli zake binafsi; (b) unafanywa kwa mujibu wa masharti ya sheria yoyote au amri ya mahakama; (c) unafanyika kwa madhumuni ya ulinzi na usalama wa Taifa na maslahi ya umma; 30

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents