Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (d) unafanyika kwa madhumuni ya kuzuia au kubaini uhalifu; (e) unafanyika kwa lengo la kubaini au kuzuia ukwepaji wa kodi; (f) unafanyika katika ukaguzi wa ubadhirifu wa fedha za umma; au (g) ni kwa madhumuni ya upekuzi kwa ajili ya uteuzi katika nafasi ya utumishi wa umma. (3) Waziri anaweza kuanisha mazingira mengine ambayo yanaweza kuondolewa katika mawanda ya masharti ya Sheria hii na masharti mengine kuhusu utekelezaji wa kifungu hiki. Amri ya uhifadhi 59.-(1) Tume inaweza kuomba amri ya mahakama kwa ajili ya uhifadhi wa haraka wa taarifa binafsi yoyote, ikijumuisha taarifa binafsi zinazopita katika mfumo, endapo kuna sababu za msingi kuwa taarifa hizo zina hatari ya kupotea au kubadilishwa. (2) Endapo mahakama itajiridhisha, chini ya kifungu kidogo cha (1), kuwa amri inaweza kutolewa chini ya kifungu kidogo hiki, itatoa amri ya uhifadhi inayoainisha kipindi kisichozidi siku tisini ambapo amri hiyo itatekelezwa. (3) Mahakama inaweza, kwa maombi ya Tume, kuongeza muda ulioainishwa katika kifungu kidogo cha (2) kwa muda ambao mahakama itaona inafaa. Makosa ya ufichuaji wa taarifa binafsi kinyume cha sheria 60.-(1) Mkusanyaji ambaye, bila sababu za msingi, atafichua taarifa binafsi kwa njia yoyote ambayo haiendani na madhumuni ambayo taarifa hiyo imekusanywa anatenda kosa. (2) Mchakataji ambae, bila sababu ya msingi, atafichua taarifa binafsi iliyochakatwa na mchakataji bila idhini ya awali ya mkusanyaji anatenda kosa. (3) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (4), mtu ambaye(a) atapata taarifa binafsi, au atapata taarifa yoyote inayojumuisha taarifa binafsi, bila idhini ya mkusanyaji au mchakataji ambaye anahifadhi taarifa hiyo; au 31

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents