Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
kukamatwa kwa vifaa vyake vyenye taarifa binafsi
vilivyohusika katika kutenda kosa.
Kanuni
64.-(1) Waziri anaweza kutengeneza kanuni kwa ajili
ya utekelezaji wa masharti ya Sheria hii.
(2) Bila kujali ujumla wa kifungu kidogo cha (1),
kanuni zitakazotengenezwa chini ya kifungu hiki zinaweza
kuainisha(a) mazingira ambayo yataondolewa katika
mawanda ya masharti ya Sheria hii;
(b) taratibu za usajili chini ya Sheria hii;
(c) majukumu ya afisa ulinzi wa taarifa
kuhusiana na ulinzi wa taarifa binafsi;
(d) majukumu ya mwakilishi wa mkusanyaji
wakati wa kufanya kazi za ukusanyaji na
uchakataji kwa niaba ya mkusanyaji;
(e) taratibu za utekelezaji wa haki chini ya Sheria
hii;
(f) taratibu za uwasilishaji wa malalamiko chini
ya Sheria hii;
(g) masharti ya uchakataji wa taarifa binafsi
nyeti;
(h) viwango sahihi vinavyohusiana na usalama
wa taarifa vinavyopaswa kuzingatiwa na
wakusanyaji;
(i) ada mbalimbali kuhusiana na shughuli za
utekelezaji wa masharti ya Sheria hii;
(j) taratibu za uhifadhi na uteketezaji wa taarifa
binafsi zinazohifadhiwa na wakusanyaji;
(k) aina ya uchakataji na mazingira ambayo
usafirishaji wa taarifa binafsi kwenda nje ya
nchi hautaruhusiwa;
(l) jambo lolote ambalo ni muhimu au linafaa
kwa ajili ya utekelezaji mzuri wa masharti ya
Sheria hii.
Kanuni za
maadili ya
ulinzi wa taarifa
binafsi
65.-(1) Kila mkusanyaji atapaswa kutengeneza kanuni
za maadili au sera kwa ajili ya ulinzi wa taarifa binafsi
zitakazobainisha
maadili
na
miiko
inayopaswa
kuzingatiwa wakati wa ukusanyaji au uchakataji wa taarifa
33
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents