Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 _______ JEDWALI ________ (Limetengenezwa chini ya kifungu cha 8(6)) TARATIBU ZA BODI Muda wa wajumbe kushika nafasi 1.-(1) Muda wa wajumbe wa Bodi kushika nafasi utakuwa kama ifuatavyo: (a) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti - miaka minne; na (b) wajumbe wengine - miaka mitatu. (2) Kila mjumbe anaweza kuteuliwa tena kwa muhula mmoja zaidi na baada ya muhula huo kuisha, hatastahili kuteuliwa tena. (3) Mjumbe yeyote anaweza kujiuzulu wakati wowote kwa kutoa notisi ya maandishi kwa mamlaka ya uteuzi na atakoma kuwa mjumbe kuanzia tarehe iliyoainishwa katika notisi au ikiwa hakuna tarehe iliyoainishwa, kuanzia tarehe ya kupokelewa kwa notisi na mamlaka ya uteuzi. Ukomo wa wajumbe 2. Mjumbe wa Bodi anaweza wakati wowote kukoma kuwa mjumbe kutokana na sababu zifuatazo: (a) kupoteza uwezo wa kutekeleza majukumu yake kutokana na ugonjwa wa mwili au akili; (b) tabia mbaya au utovu wa nidhamu kwa namna ambayo italeta au kuwa na uwezekano wa kuleta sifa mbaya kwa Bodi; (c) kutohudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bodi bila kutoa taarifa; au (d) kujiuzulu; na (e) kifo. Kutokuhudhuria vikao vya Bodi 3.-(1) Endapo mjumbe yeyote hatahudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bodi bila taarifa, Bodi inaweza kuishauri mamlaka ya uteuzi kuhusu suala hilo na mamlaka ya uteuzi inaweza kutengua uteuzi wa mjumbe huyo na kuteua mjumbe mwingine badala yake. (2) Iwapo mjumbe yeyote kwa sababu ya ugonjwa, udhaifu au kutokuwepo katika Jamhuri ya Muungano hawezi kuhudhuria kikao chochote cha Bodi, Waziri anaweza kuteua mjumbe wa muda badala yake na mjumbe huyo wa muda atakoma kushika wadhifa huo baada ya mjumbe husika kurejea katika nafasi yake. Shughuli za Bodi kutobatilishwa kwa sababu ya kasoro 4. Shughuli za Bodi hazitakuwa batili kwa sababu ya kasoro yoyote katika uteuzi wa mjumbe yeyote au kwa kigezo kuwa mjumbe yeyote wakati wa uteuzi hakuwa na sifa au hakustahili kuteuliwa. Vikao vya Bodi 5.-(1) Bodi itakutana kila robo mwaka kwa nyakati na mahali itakapoona inafaa kwa ajili ya shughuli zake. (2) Mwenyekiti au pale ambapo hayupo, Makamu Mwenyekiti, anaweza kuitisha kikao maalum au kikao cha dharura cha Bodi. (3) Kikao cha kawaida cha Bodi kitaitishwa na Mwenyekiti na taarifa inayobainisha mahali, tarehe na muda wa kikao itatolewa kwa 35

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents