Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 kukamatwa kwa vifaa vyake vyenye taarifa binafsi vilivyohusika katika kutenda kosa. Kanuni 64.-(1) Waziri anaweza kutengeneza kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Sheria hii. (2) Bila kujali ujumla wa kifungu kidogo cha (1), kanuni zitakazotengenezwa chini ya kifungu hiki zinaweza kuainisha(a) mazingira ambayo yataondolewa katika mawanda ya masharti ya Sheria hii; (b) taratibu za usajili chini ya Sheria hii; (c) majukumu ya afisa ulinzi wa taarifa kuhusiana na ulinzi wa taarifa binafsi; (d) majukumu ya mwakilishi wa mkusanyaji wakati wa kufanya kazi za ukusanyaji na uchakataji kwa niaba ya mkusanyaji; (e) taratibu za utekelezaji wa haki chini ya Sheria hii; (f) taratibu za uwasilishaji wa malalamiko chini ya Sheria hii; (g) masharti ya uchakataji wa taarifa binafsi nyeti; (h) viwango sahihi vinavyohusiana na usalama wa taarifa vinavyopaswa kuzingatiwa na wakusanyaji; (i) ada mbalimbali kuhusiana na shughuli za utekelezaji wa masharti ya Sheria hii; (j) taratibu za uhifadhi na uteketezaji wa taarifa binafsi zinazohifadhiwa na wakusanyaji; (k) aina ya uchakataji na mazingira ambayo usafirishaji wa taarifa binafsi kwenda nje ya nchi hautaruhusiwa; (l) jambo lolote ambalo ni muhimu au linafaa kwa ajili ya utekelezaji mzuri wa masharti ya Sheria hii. Kanuni za maadili ya ulinzi wa taarifa binafsi 65.-(1) Kila mkusanyaji atapaswa kutengeneza kanuni za maadili au sera kwa ajili ya ulinzi wa taarifa binafsi zitakazobainisha maadili na miiko inayopaswa kuzingatiwa wakati wa ukusanyaji au uchakataji wa taarifa 33

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents