Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
usajili
Tume chini ya Sehemu hii anaweza kuwasilisha rufaa kwa
njia ya maandishi kwa Waziri.
Usajili wa
taasisi za umma
21. Mara baada ya kuanza kutumika kwa Sheria hii,
taasisi za umma zinazoshughulika na ukusanyaji na
uchakataji wa taarifa binafsi zitachukuliwa kuwa
zimesajiliwa chini ya Sheria hii na zitapaswa kuzingatia
masharti ya Sheria.
SEHEMU YA NNE
UKUSANYAJI, UTUMIAJI, UFICHUAJI NA UHIFADHI WA TAARIFA
BINAFSI
Ukusanyaji wa
taarifa binafsi
22.-(1) Sehemu hii itatumika kwa(a) ukusanyaji na uchakataji wowote wa taarifa binafsi
uliofanywa kwa taarifa yote au sehemu ya taarifa
hiyo kwa njia ya kielektroniki au isiyo ya
kielektroniki;
(b) uchakataji wa taarifa binafsi unaofanywa katika
utekelezaji wa majukumu ya mkusanyaji anayeishi
katika Jamhuri ya Muungano au katika sehemu
ambayo sheria za Jamhuri ya Muungano zinatumika
kwa mujibu wa sheria za kimataifa;
(c) uchakataji wa taarifa binafsi unaofanywa na
mkusanyaji au mchakataji anayeishi nje ya Jamhuri
ya Muungano, ikiwa uchakataji huo umefanyika
nchini na sio kwa madhumuni ya kupitisha nchini
taarifa binafsi kwenda nchi nyingine.
(2) Mkusanyaji atakusanya taarifa binafsi iwapo(a) taarifa binafsi inakusanywa kwa madhumuni
halali yanayohusiana na kazi ya mkusanyaji; na
(b) ukusanyaji wa taarifa binafsi ni muhimu au
unatokana, au kuhusiana moja kwa moja, na
madhumuni halali.
(3) Mkusanyaji hatakusanya taarifa binafsi kwa
njia zisizo halali.
Chanzo na
utoaji wa taarifa
binafsi
23.-(1) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (3),
mkusanyaji atakusanya taarifa binafsi moja kwa moja
kutoka kwa mhusika wa taarifa.
(2) Kabla ya kukusanya taarifa binafsi, mkusanyaji
atahakikisha kuwa mhusika13
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents