Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (a) anatambua madhumuni ya ukusanyaji wa taarifa binafsi; (b) anafahamu kuwa ukusanyaji wa taarifa binafsi ni kwa madhumuni yaliyoidhinishwa; na (c) anawafahamu wapokeaji wa taarifa binafsi waliokusudiwa. (3) Mkusanyaji hatalazimika kuzingatia kifungu kidogo cha (1) iwapo(a) taarifa binafsi husika zimekwisha wekwa wazi; (b) mhusika wa taarifa binafsi ameidhinisha taarifa zake kukusanywa kutoka kwa mtu mwingine; (c) utekelezaji wake umeshindikana katika mazingira husika; (d) kutokutekelezwa kwake ni kwa mujibu wa sheria; na (e) utekelezaji wake unaweza kuathiri madhumuni ya ukusanyaji. Usahihi wa taarifa binafsi 24. Kwa kuzingatia madhumuni ambayo taarifa binafsi zinapendekezwa kutumika, mkusanyaji ambaye ana taarifa binafsi hatatumia taarifa hizo kwa mazingira yaliyopo bila kuchukua hatua zinazohakikisha kuwa taarifa hizo zimekamilika, ziko sahihi, zinaendana na maudhui na hazipotoshi. Taarifa binafsi kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa 25.-(1) Taarifa binafsi zilizokusanywa kwa mujibu wa Sheria hii zitatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa. (2) Endapo mkusanyaji ana taarifa binafsi ambazo amekusanya kwa madhumuni maalum, anaweza kutumia taarifa hizo kwa madhumuni mengine iwapo(a) mhusika ameidhinisha matumizi ya taarifa binafsi kwa dhumuni hilo; (b) matumizi ya taarifa binafsi kwa dhumuni hilo yameidhinishwa au kuhitajika kisheria; (c) dhumuni ambalo taarifa binafsi imetumika linahusiana moja kwa moja na dhumuni la ukusanyaji wa taarifa hiyo; (d) taarifa binafsi inatumika(i) kwa namna ambayo mhusika hatambuliki; au (ii) kwa madhumuni ya takwimu au utafiti na 14

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents