Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 haitachapishwa kwa namna ambayo inaweza kumtambulisha mhusika; (e) mkusanyaji anaamini kwa sababu za msingi kuwa matumizi ya taarifa binafsi kwa hayo madhumuni mengine ni muhimu ili kuzuia au kupunguza madhara kwa uhai au afya ya mtu husika au mtu mwingine, au kwa afya au usalama wa jamii; au (f) matumizi ya taarifa binafsi kwa hayo madhumuni mengine ni muhimu katika uzingatiwaji wa sheria. Mipaka ya ufichuaji wa taarifa binafsi 26. Endapo mkusanyaji ana taarifa binafsi, hatafichua taarifa hizo kwa mtu tofauti na mhusika wa taarifa, isipokuwa kwa mazingira yaliyoainishwa katika kifungu cha 25. Usalama wa taarifa binafsi 27.-(1) Mkusanyaji na wawakilishi wake watahakikisha kuwa taarifa binafsi zinalindwa, kwa kuchukua hatua za kiusalama zinazohitajika kwa usalama wa taarifa hizo dhidi ya upotevu wa kizembe au uteketezaji, ubadilishaji, upatikanaji au uchakataji wa taarifa binafsi bila idhini. (2) Hatua za kiusalama zitakazochukuliwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) zinapaswa kuhakikisha kiwango cha usalama kinachohitajika kwa kuzingatia(a) mabadiliko ya kiteknolojia na gharama za kutekeleza hatua hizo; na (b) aina ya taarifa binafsi inayopaswa kulindwa na madhara yanayoweza kutokea kwa mhusika wa taarifa. (3) Mkusanyaji au mchakataji atapaswa kuteua afisa ulinzi wa taarifa binafsi atakayehakikisha hatua za kiudhibiti na za kiusalama zinachukuliwa ili kulinda taarifa binafsi zinazokusanywa au kuchakatwa. (4) Utekelezaji wa shughuli za mchakataji utasimamiwa kwa mkataba utakaoainisha uhusiano kati ya mchakataji na mkusanyaji kwa namna ambayo mchakataji atatekeleza shughuli zake kwa maelekezo ya mkusanyaji, 15

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents