Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
(c) ni kutokana na ridhaa iliyotolewa na mhusika
wa taarifa.
Haki ya fidia
37.-(1) Mhusika wa taarifa atakayepata madhara kwa
sababu za ukiukwaji wa masharti ya Sheria hii uliofanywa
na mkusanyaji au mchakataji atakuwa na haki ya kulipwa
fidia kutoka kwa mkusanyaji au mchakataji kutokana na
madhara hayo.
(2) Mhusika wa taarifa ambaye haki zake
zimevunjwa kwa sababu ya ukiukwaji wa masharti yoyote
ya Sheria hii atakuwa na haki ya kulipwa fidia kutoka kwa
mkusanyaji au mchakataji ikiwa(a) mlalamikaji ndiye mhusika wa taarifa
aliyeathiriwa au mwakilishi wa mhusika wa
taarifa ikiwa mhusika ni mtoto au mtu asiye na
akili timamu;
(b) haki za mhusika wa taarifa zimevunjwa kwa
sababu ya ukiukwaji huo; na
(c) athari hizo zinahusiana na uchakataji wa taarifa
binafsi kinyume na masharti ya Sheria hii.
(3) Endapo Tume itajiridhisha na maombi ya
mhusika wa taarifa(a) kwamba amepata madhara kwa sababu ya
ukiukwaji wa masharti ya Sheria hii uliofanywa
na mkusanyaji au mchakataji kuhusiana na
taarifa binafsi yoyote, katika mazingira
yanayompatia haki ya kulipwa fidia chini ya
kifungu hiki; na
(b) kwamba kuna hatari kubwa ya ukiukwaji zaidi
kuhusiana na taarifa binafsi husika katika
mazingira hayo,
Tume inaweza kuamuru kurekebishwa, kuzuiwa, kufutwa
au kuharibiwa kwa taarifa hizo.
(4) Tume, pale ambapo imetoa amri chini ya
kifungu kidogo cha (3) na endapo itaona kuwa ni busara,
inaweza kumuamuru mkusanyaji au mchakataji
kuwajulisha wahusika wengine ambao wamepatiwa taarifa
binafsi kuhusu marekebisho, zuio, ufutaji au uharibifu wa
taarifa hizo.
(5) Katika kuamua endapo ni sahihi kuhitaji
22
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents