Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 Notisi ya utekelezaji 45.-(1) Pale ambapo Tume imeridhika kuwa mtu ameshindwa kuzingatia kifungu chochote cha Sheria hii, Tume inaweza kutoa notisi ya utekelezaji kwa mtu huyo ikimtaka kuchukua hatua za kurekebisha mapungufu ndani ya kipindi kitakachoainishwa katika notisi. (2) Notisi ya utekelezaji itakayotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1)(a) itaainisha kifungu cha Sheria hii ambacho kimekiukwa; (b) itaainisha hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kukabiliana au kuondoa tatizo husika; (c) itabainisha kipindi ambacho hatua husika zitapaswa kutekelezwa ambacho hakitapungua siku ishirini na moja; na (d) itaeleza haki ya kukata rufaa. Notisi ya adhabu 46.-(1) Pale ambapo Tume itajiridhisha kuwa mtu ameshindwa au anashindwa kuzingatia notisi ya utekelezaji iliyotolewa chini ya kifungu cha 45, Tume inaweza kutoa notisi ya adhabu inayomtaka mtu kulipa kwa Tume faini ya kiasi kitakachoainishwa kwenye notisi. (2) Katika kuamua iwapo inaweza kutoa notisi ya adhabu kwa mtu na kuamua kiasi cha adhabu, Tume itapaswa, kadiri itakavyoona muhimu, kuzingatia(a) aina na uzito wa ukiukwaji, na muda ambao ukiukwaji huo umekuwa ukiendelea; (b) endapo ukiukwaji umefanywa kwa nia ovu au uzembe; (c) hatua yoyote iliyochukuliwa na mkusanyaji au mchakataji ili kupunguza madhara waliyoyapata wahusika wa taarifa zikiwemo hatua za kiufundi na za kiutawala; (d) ukiukwaji aliowahi kufanya mkusanyaji au mchakataji awali; (e) kiwango cha ushirikiano alichoonesha kwa Tume kwa lengo la kurekebisha ukiukwaji na kupunguza athari hasi za ukiukwaji zinazoweza kujitokeza; (f) aina ya taarifa binafsi zilizoathiriwa na ukiukwaji; 26

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents