Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (g) namna ambayo Tume ilifahamu kuhusu ukiukwaji, ikijumuisha endapo mkusanyaji au mchakataji aliifahamisha Tume; (h) kiwango ambacho mkusanyaji au mchakataji alizingatia notisi za utekelezaji na notisi za adhabu zilizowahi kutolewa awali; (i) uzingatiaji wa kanuni za maadili au vigezo na masharti ya usajili; (j) endapo adhabu itakuwa na ufanisi; na (k) kigezo kingine chochote kinachoweza kutumika kuongeza au kupunguza adhabu, ikiwa ni pamoja na faida za kifedha alizozipata au hasara alizosababisha, moja kwa moja au vinginevyo, kutokana na ukiukwaji huo. Faini za kiutawala 47. Kiwango cha juu cha adhabu kinachoweza kutolewa na Tume katika notisi ya adhabu kuhusiana na ukiukwaji wa masharti ya Sheria hii, ni shilingi milioni mia moja. Marejeo ya uamuzi 48.-(1) Tume baada ya kuombwa au kwa utashi wake yenyewe inaweza kufanya marejeo ya uamuzi na maelekezo yake iliyoyatoa kwa mujibu wa masharti ya Sehemu hii. (2) Baada ya kufanya marejeo kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) Tume inaweza kutengua, kubadilisha au kusitisha uamuzi au maelekezo yake iliyoyatoa awali. Haki ya rufaa 49. Mtu ambaye hataridhika na hatua yoyote ya kiutawala itakayochukuliwa na Tume, ikiwa ni pamoja na maelekezo yaliyotolewa katika notisi ya utekelezaji au adhabu iliyotolewa katika notisi ya adhabu, anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu. Malipo ya fidia 50.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 37, Tume inaweza pamoja na adhabu nyingine zilizotolewa chini ya Sheria hii, kumuamuru mkusanyaji au mchakataji aliyesababisha madhara kwa mhusika wa taarifa kutokana na ukiukwaji wa masharti ya Sheria hii kulipa fidia kwa mhusika wa taarifa. 27

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents