Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
(2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1)(a) mkusanyaji anayehusika katika uchakataji wa
taarifa binafsi atawajibika kwa madhara
yatakayotokana na uchakataji huo; na
(b) mchakataji anayehusika na uchakataji wa
taarifa binafsi atawajibika kwa madhara
yatakayotokana na uchakataji huo ikiwa(i) hajatekeleza wajibu ulioelekezwa
mahsusi kwa wachakataji chini ya
Sheria hii; au
(ii) ametenda kinyume na maelekezo halali
ya mkusanyaji.
(3) Mkusanyaji au mchakataji hatawajibika kwa
namna iliyoainishwa katika kifungu kidogo cha (2) ikiwa
mkusanyaji au mchakataji huyo atathibitisha kuwa
hakuhusika kwa namna yoyote katika tukio lililosababisha
madhara.
(4) Katika sehemu hii, "madhara" yanajumuisha
upotevu wa fedha na madhara yasiyohusisha upotevu wa
fedha.
SEHEMU YA NANE
MASHARTI YA FEDHA
Vyanzo vya
fedha za Tume
51. Fedha za Tume zitajumuisha(a) kiasi cha fedha ambacho kinaweza kutengwa na
Bunge;
(b) fedha zitakazopatikana kutokana na huduma,
ushauri au malipo mengine;
(c) fedha zitakazotokana na michango, zawadi au
ruzuku;
(d) mikopo; na
(e) mapato mengine yatakayotokana na utendaji wa
shughuli za Tume chini ya Sheria hii.
Usimamizi wa
fedha
52. Fedha za Tume zitasimamiwa na Bodi kwa mujibu
wa sheria za fedha na zitatumika kugharamia matumizi
yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu ya Tume chini
ya Sheria hii
28
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents