Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 Makadirio ya mapato na matumizi na udhibiti wa fedha 53.-(1) Mkurugenzi Mkuu atapaswa, katika kipindi kisichopungua miezi mitatu kabla ya mwisho wa kila mwaka wa fedha, kuandaa na kuwasilisha katika Bodi ili kuidhinisha, bajeti inayojumuisha makadirio ya mapato na matumizi kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1), Tume itawasilisha nakala ya bajeti kwa Waziri kwa ajili ya kuidhinishwa. (3) Waziri anaweza kuitaka Tume kufanya marekebisho katika bajeti ikiwa kwa maoni yake bajeti haiwakilishi makadirio sahihi na ya kuridhisha ya mapato na matumizi. Matumizi ya fedha 54. Matumizi hayatafanyika kutoka kwenye fedha za Tume isipokuwa kama matumizi hayo ni sehemu ya matumizi yaliyoidhinishwa na Bodi chini ya kifungu cha 53(1) kuhusiana na mwaka wa fedha ambao matumizi yaliidhinishwa. Makadirio ya nyongeza 55.-(1) Bodi inaweza, wakati wowote kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha husika, kuandaa na kuwasilisha kwa Waziri kwa ajili ya kuidhinishwa makadirio yoyote ya nyongeza ya makadirio ya mwaka husika. (2) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1), Mkurugenzi Mkuu anaweza, pale ambapo dharura imetokea katika utekelezaji wa majukumu ya Tume, kufanya matumizi ambayo hayajaidhinishwa na Bodi ambapo Mkurugenzi Mkuu atalazimika, ndani ya miezi mitatu inayofuata, kuomba idhini ya Bodi kwa matumizi hayo. Akaunti na ukaguzi 56.-(1) Tume itaweka vitabu vya hesabu na kutunza kumbukumbu sahihi za shughuli zake kwa mujibu wa viwango vya uhasibu. (2) Tume itapaswa, ndani ya miezi sita baada ya mwisho wa kila mwaka wa fedha, kuandaa ripoti ya utekelezaji wa majukumu yake katika mwaka huo wa fedha, na nakala moja ya ripoti hiyo pamoja na nakala ya hesabu zilizokaguliwa zitawasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. 29

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents