Na 11
Sura ya 286
Taarifa za kila
mwaka na
mikataba ya
utekelezaji
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
(3) Hesabu za Tume zitakaguliwa na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali au mtu mwingine
aliyesajiliwa kama mkaguzi chini ya Sheria ya Usajili wa
Wakaguzi na Wahasibu aliyeteuliwa na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa dhumuni hilo.
57.-(1) Ndani ya muda wa miezi miwili baada ya
kupokea hesabu zilizokaguliwa na taarifa ya mkaguzi wa
hesabu, Mkurugenzi Mkuu atapaswa kuwasilisha kwa
Waziri taarifa ya mwaka husika ikijumuisha(a) nakala ya hesabu zilizokaguliwa pamoja na
taarifa ya mkaguzi kwenye akaunti hizo;
(b) taarifa ya utekelezaji wa malengo muhimu na
taarifa nyingine yoyote inayohusiana na
utekelezaji wa malengo hayo;
(c) taarifa ya uendeshaji wa Tume katika mwaka
wa fedha husika; na
(d) taarifa nyingine kama ambavyo Waziri anaweza
kuhitaji.
(2) Waziri atawasilisha Bungeni nakala ya taarifa
ya mwaka ya Tume ndani ya miezi miwili au katika
mkutano wa Bunge unaofuata.
SEHEMU YA TISA
MASHARTI MENGINEYO
Mazingira
yanayoondolew
a katika
mawanda ya
Sheria hii
58.-(1) Hakuna chochote katika kifungu hiki
kitakachomuondolea mkusanyaji au mchakataji wajibu wa
kuzingatia misingi ya sheria katika ukusanyaji na
uchakataji wa taarifa binafsi na uchukuaji wa hatua
muhimu katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa taarifa
binafsi alizonazo.
(2) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1), uchakataji
wa taarifa binafsi unaweza kuondolewa katika mawanda ya
masharti ya Sheria hii ikiwa uchakataji huo(a) unafanywa na mhusika wa taarifa katika
shughuli zake binafsi;
(b) unafanywa kwa mujibu wa masharti ya sheria
yoyote au amri ya mahakama;
(c) unafanyika kwa madhumuni ya ulinzi na
usalama wa Taifa na maslahi ya umma;
30
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents