Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
(d) unafanyika kwa madhumuni ya kuzuia au
kubaini uhalifu;
(e) unafanyika kwa lengo la kubaini au kuzuia
ukwepaji wa kodi;
(f) unafanyika katika ukaguzi wa ubadhirifu wa
fedha za umma; au
(g) ni kwa madhumuni ya upekuzi kwa ajili ya
uteuzi katika nafasi ya utumishi wa umma.
(3) Waziri anaweza kuanisha mazingira mengine
ambayo yanaweza kuondolewa katika mawanda ya
masharti ya Sheria hii na masharti mengine kuhusu
utekelezaji wa kifungu hiki.
Amri ya
uhifadhi
59.-(1) Tume inaweza kuomba amri ya mahakama kwa
ajili ya uhifadhi wa haraka wa taarifa binafsi yoyote,
ikijumuisha taarifa binafsi zinazopita katika mfumo,
endapo kuna sababu za msingi kuwa taarifa hizo zina
hatari ya kupotea au kubadilishwa.
(2) Endapo mahakama itajiridhisha, chini ya
kifungu kidogo cha (1), kuwa amri inaweza kutolewa chini
ya
kifungu kidogo hiki, itatoa amri ya uhifadhi
inayoainisha kipindi kisichozidi siku tisini ambapo amri
hiyo itatekelezwa.
(3) Mahakama inaweza, kwa maombi ya Tume,
kuongeza muda ulioainishwa katika kifungu kidogo cha
(2) kwa muda ambao mahakama itaona inafaa.
Makosa ya
ufichuaji wa
taarifa binafsi
kinyume cha
sheria
60.-(1) Mkusanyaji ambaye, bila sababu za msingi,
atafichua taarifa binafsi kwa njia yoyote ambayo haiendani
na madhumuni ambayo taarifa hiyo imekusanywa anatenda
kosa.
(2) Mchakataji ambae, bila sababu ya msingi,
atafichua taarifa binafsi iliyochakatwa na mchakataji bila
idhini ya awali ya mkusanyaji anatenda kosa.
(3) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (4), mtu
ambaye(a) atapata taarifa binafsi, au atapata taarifa yoyote
inayojumuisha taarifa binafsi, bila idhini ya
mkusanyaji au mchakataji ambaye anahifadhi
taarifa hiyo; au
31
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents