Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (b) atafichua taarifa binafsi kwa mtu mwingine, anatenda kosa. (4) Mtu atakayeuza taarifa binafsi ambayo imepatikana kwa ukiukwaji wa kifungu kidogo cha (1) anatenda kosa. (5) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (4), tangazo linaloonesha kwamba taarifa binafsi inauzwa au inaweza kuuzwa itachukuliwa kuwa ni ofa ya kuuza taarifa binafsi. (6) Mtu atakayebainika kutenda kosa chini ya kifungu hiki atakapotiwa hatiani atawajibika(a) ikiwa ni mtu binafsi, kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi milioni ishirini au kifungo kwa kipindi kisichozidi miaka kumi au vyote kwa pamoja; na (b) ikiwa ni kampuni au shirika, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja na isiyozidi shilingi bilioni tano. Makosa ya uharibifu, ufutaji, ufichaji au ubadilishaji wa taarifa binafsi kinyume cha sheria 61. Mtu ambaye ataharibu, atafuta, atapotosha, ataficha au kubadilisha taarifa binafsi kinyume cha sheria anatenda kosa na atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi milioni kumi au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja. Makosa yanayotendwa na kampuni au shirika 62. Pale ambapo kosa chini ya Sheria hii limetendwa na kampuni au shirika, kampuni au shirika hilo na kila afisa wa shirika ambaye kwa kujua na kwa makusudi anaidhinisha au kuruhusu ukiukaji atawajibika kwa kosa hilo. Adhabu ya jumla 63.-(1) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria hii, anatenda kosa na pale ambapo hakuna adhabu mahususi iliyoainishwa, atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja. (2) Baada ya mtu kutiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria hii, mahakama inaweza kuamuru 32

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents