Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
wajumbe si chini ya siku kumi kabla ya tarehe ya kikao na endapo
Mwenyekiti hawezi kuitisha kikao kwa sababu ya ugonjwa au sababu
nyingine yoyote au hayupo katika Jamhuri ya Muungano, Makamu
Mwenyekiti anaweza kuitisha kikao hicho.
(4) Bodi inaweza kuendelea na shughuli zake bila kujali kuwa
nafasi yoyote ya ujumbe iko wazi.
Mgongano wa
maslahi
6.-(1) Pale ambapo mjumbe wa Bodi wakati wowote ana mgongano
wa maslahi kuhusiana na(a) suala lolote lililo mbele ya Bodi kwa ajili ya kujadiliwa au
kuamuliwa;
(b) jambo lolote ambalo Bodi inaweza kutarajia kuwa linaweza
kufika mbele yake kwa ajili ya kujadiliwa au kuamuliwa,
mjumbe atafichua mara moja mgongano wa maslahi kwa wajumbe
wengine wa Bodi na kuacha kushiriki katika, au kuendelea kuwa sehemu
ya, kujadili au kuamua jambo hilo.
(2) Iwapo Bodi itafahamu kwamba mjumbe ana mgongano wa
maslahi kuhusiana na jambo lolote lililo mbele ya Bodi, itamuelekeza
mjumbe huyo kutoshiriki au kutoendelea kushiriki katika kujadili au
kuamua suala hilo.
(3) Mjumbe wa Bodi atachukuliwa kuwa amekiuka masharti ya
aya ndogo ya (1) ikiwa(a) atashindwa bila sababu za msingi kuweka wazi maslahi
yake kama anavyotakiwa; au
(b) kwa kujua atatoa tamko la uongo au la kupotosha ambalo
lina athari katika uamuzi,
mtu huyo atakuwa anatenda kosa na atapaswa kujiuzulu katika wadhifa
wake.
Mwaliko wa
mtaalamu
7. Bodi inaweza kumwalika mtu yeyote ambaye si mjumbe kushiriki
katika mijadala ya Bodi na kutoa utaalam kama Bodi itakavyohitaji, lakini
mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura.
Akidi
8. Akidi katika kikao chochote cha Bodi itakuwa zaidi ya nusu ya
wajumbe wa Bodi.
Muhtasari wa
vikao
9. Muhtasari wa kila kikao cha Bodi utahifadhiwa na kuthibitishwa
na Bodi katika kikao kitakachofuata.
Uamuzi wa Bodi
10. Uamuzi wa Bodi katika suala lolote utakuwa kwa wingi wa kura
za wajumbe waliopo na pale ambapo kura hizo zitalingana, Mwenyekiti
atakuwa na kura ya turufu.
Bodi kuendesha
taratibu zake
11. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, Bodi itakuwa na mamlaka
ya kusimamia taratibu zake kuhusiana na vikao na ufanyaji wa shughuli
zake.
36
Select target paragraph3
Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents