Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 50 (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja. Ponografia za watoto 13. -(1) Mtu yeyote(a) hatachapisha ponografia za watoto kwa kupitia mfumo wa kompyuta; au (b) hatatoa au hatawezesha upatikanaji au kuonyeshwa kwa ponografia za watoto kwa kupitia mfumo wa kompyuta. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni hamsini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja. (3) Mtu aliyetiwa hatiani kwa kosa chini ya kifungu hiki, pamoja na adhabu nyingine yoyote, anaweza kuamriwa kumlipa fidia mtu ambaye ameathirika na kosa hilo. Ponografia 14.-(1) Mtu hatachapisha au kusababisha kuchapishwa kupitia katika mfumo wa kompyuta(a) ponografia; au (b) ponografia yoyote iliyo ya kiasherati au chafu. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, iwapo ni uchapishaji kuhusiana na-

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos