No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 60 (iii) shauri lolote lililopo mahakamani au ambalo linaweza kufunguliwa kuhusiana na uchunguzi wowote. (6 ) Katika kifungu hiki “eneo” inajumuisha ardhi, majengo au chombo cha usafiri baharini au ndege. Utoaji data 32. -(1) Endapo data inahitajika kuwekwa wazi kwa madhumuni ya uchunguzi wa kijinai au kuendeshwa kwa kesi mahakamani, askari polisi mfawidhi wa kituo au afisa mtekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa kituo anaweza kutoa amri kwa mtu yeyote mwenye data hiyo kumtaka kutoa data hiyo. (2 ) Amri iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha ( 1) atapewa afisa utekelezaji sheria ambaye ataiwasilisha kwa mtu huyo mwenye data. (3) Endapo utoaji wa data chini ya kifungu kidogo cha ( 1) hauwezekani, afisa utekelezaji sheria anaweza kuiomba mahakama kutoa amri inayotamka: (a) mtu yeyote kuwasilisha data iliyoainishwa ambayo mtu huyo anaimiliki au iliyo chini ya uangalizi; au (b) mtoa huduma anayetoa huduma zake, kuwasilisha zinazohusu huduma hiyo zilizo kwenye umiliki au uangalizi wake. (4) Iwapo kitu chochote kinachohusiana na upelelezi kinajumuisha data iliyohifadhiwa kwenye mfumo wa kompyuta au kwenye kifaa, amri itachukuliwa kumtaka mtu huyo kutoa au kuruhusu upatikanaji wa data hiyo katika namna ambayo inasomeka na inayoweza kuondolewa. Utunzaji data wa dharura 33. (1) Endapo askari polisi Mkuu wa kituo au afisa utekelezaji wa sheria anazo sababu za kuamini kuwa data kompyuta ambayo inahitajika kwa madhumuni ya uchunguzi inaweza kupotea au kubadilishwa, anaweza kutoa amri itakayomtaka mtu mwenye uangalizi au umiliki wa kifaa au data kompyuta hiyo kuitunza kwa kipindi kisichozidi siku kumi na nne.

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos