Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao kutumikia kifungo kwa kipindi mmoja au vyote kwa pamoja. 2015 48 kisichopungua mwaka Ujasusi data Sura ya 47 8. -(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria ya Usalama wa Taifa, mtu hataingilia na kujipatia data kompyuta iliyokingwa dhidi ya uingiaji bila idhini. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au yoyote iliyokubwa, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano au vyote kwa pamoja. Kuingilia mfumo kinyume cha sheria 9. Mtu ambaye, kwa makusudi na kinyume cha sheria anazuia au anaingilia(a) utendaji kazi wa mfumo wa kompyuta; (b) matumizi au uendeshaji wa mfumo wa kompyuta, atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni mbili au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. Kifaa kisicho halali 10. -(1) Mtu hatajishughulisha na, au kumiliki, kinyume cha sheria(a) kifaa, ikijumuisha programu ya kompyuta iliyotengenezwa au inayotumiwa kwa madhumuni ya kutenda kosa; (b) namba ya siri ya kompyuta, ishara ya kuingilia au data inayofanana na hiyo ambayo inaweza kutumika na

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos