51 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 (a) ponografia, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja; au (b) ponografia iliyo ya kiasherati au chafu, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni thelathini au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka kumi au vyote kwa pamoja. Makosa yanayohusiana na utambuzi 15. -(1) Mtu hatajifanya kuwa mtu mwingine kwa kutumia mfumo wa kompyuta. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja. Kutoa taarifa za uongo 16. Mtu atakayechapisha taarifa au data katika picha, maandishi, alama au katika namna nyingine yoyote katika mfumo wa kompyuta, akijua kwamba taarifa au data ni za uongo, zinapotosha, zisizo sahihi, na kwa lengo la kudhalilisha, kutishia, kutusi au kwa naamna nyingine kudanganya umma au kuchochea utendaji wa kosa, atakuwa ametenda kosa, na akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kidungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja. Ubaguzi 17. -(1) Mtu, kwa kutumia mfumo wa kompyuta(a) hatazalisha vitu vya kibaguzi kwa madhumuni ya kuvisambaza; (b) hatatoa au kuwezesha kupatikana vitu vya kibaguzi ; au (c) hatarusha au kusambaza vitu vya kibaguzi.

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos