Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 taarifa binafsi; “nyaraka” maana yake ni njia yoyote ambayo taarifa imerekodiwa, iwe imechapishwa au ipo kwenye mkanda au filamu au kwa njia ya kielektroniki au vinginevyo na inajumuisha ramani, mchoro, picha, filamu, filamu ndogo, mkanda wa video, rekodi ya sauti au rekodi inayosomeka kwa mashine au rekodi yenye uwezo wa kuzalishwa kutoka kwa rekodi inayosomeka kwa mashine kwa njia ya vifaa au programu, au mchanganyiko wa zote mbili, vinavyotumiwa na mkusanyaji kwa madhumuni ya kutunza kumbukumbu; “rejesta” maana yake ni rejesta iliyoanzishwa na Tume kwa mujibu wa kifungu cha 15; “taarifa binafsi” maana yake ni taarifa kuhusu mtu anayetambulika ambazo zimetunzwa kwa namna yoyote, ikiwa ni pamoja na(a) taarifa binafsi zinazohusu rangi, asili ya kitaifa au kikabila, dini, umri au hali ya ndoa ya mtu binafsi; (b) taarifa binafsi zinazohusu elimu, historia ya matibabu, jinai au ajira; (c) namba yoyote ya utambulisho, alama au namna nyingine maalum inayomtambulisha mtu binafsi; (d) anwani, alama za vidole au kundi la damu la mtu binafsi; (e) jina la mtu binafsi linaloonekana katika taarifa binafsi za mtu mwingine anayehusiana naye au pale ambapo ufichuzi wa jina hilo utadhihirisha taarifa binafsi za mtu; (f) taarifa iliyotumwa kwa mkusanyaji wa taarifa binafsi na mtu, ambayo ni wazi kuwa taarifa hiyo ni binafsi au ya siri, na majibu kwa taarifa hiyo yanaweza kufichua maudhui ya taarifa ya awali, na mtazamo au maoni ya mtu mwingine yeyote kuhusu mhusika wa taarifa; “taarifa binafsi nyeti” inajumuisha(a) taarifa ya vinasaba, taarifa inayohusu watoto, taarifa inayohusu makosa, miamala ya kifedha ya mtu binafsi au hatua za kiusalama, taarifa za kibayometriki; 6

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos