Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
(e) kuwapa wahusika wa taarifa haki na nafuu
katika kulinda taarifa binafsi kutokana na
ukusanyaji na uchakataji usiofuata masharti ya
Sheria hii.
Misingi ya
ulinzi wa taarifa
binafsi
5. Mkusanyaji au mchakataji atahakikisha kwamba
taarifa binafsi(a) zinachakatwa kihalali, kwa haki na kwa uwazi;
(b) zinakusanywa kwa madhumuni mahususi,
yaliyobainishwa na halali, na taarifa hizo
hazitaendelea kuchakatwa kwa namna tofauti
na madhumuni yaliyoainishwa;
(c) zinatosheleza na ni muhimu kwa madhumuni
ya uchakataji kama ilivyokusudiwa;
(d) ni sahihi na pale inapobidi, zinaboreshwa kwa
kuchukua hatua zote muhimu kuhakikisha
taarifa binafsi zisizo sahihi zinafutwa au
kurekebishwa bila kuchelewa;
(e) zinahifadhiwa katika namna inayoruhusu
utambuzi wa mhusika wa taarifa kwa muda
usiozidi ule unaohitajika kwa madhumuni ya
uchakataji wa taarifa binafsi husika;
(f) zinachakatwa kwa kuzingatia haki za mhusika
wa taarifa;
(g) zinachakatwa kwa namna ambayo itahakikisha
usalama wa taarifa binafsi, ikijumuisha ulinzi
dhidi ya uchakataji usioruhusiwa au ulio
kinyume cha sheria na dhidi ya hasara,
uharibifu au madhara yoyote, kwa kutumia
hatua sahihi za kiufundi au za kiutawala; na
(h) hazisafirishwi nje ya mipaka ya nchi kinyume
cha masharti ya Sheria hii.
SEHEMU YA PILI
TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI
Uanzishwaji wa
Tume ya Ulinzi
wa Taarifa
Binafsi
6.-(1) Inaanzishwa Tume itakayojulikana kama Tume
ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
(2) Tume itakuwa taasisi nafsi yenye mamlaka ya
urithishaji wa kudumu na lakiri yake, na kwa jina lake
8
Seleccionar párrafo de destino3
Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos