Na 11 Katazo la uchakataji wa taarifa binafsi nyeti Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 30.-(1) Mtu hatachakata taarifa binafsi nyeti bila ridhaa ya maandishi ya mhusika wa taarifa. (2) Ridhaa chini ya kifungu kidogo cha (1) inaweza kuondolewa na mhusika wa taarifa wakati wowote na bila maelezo au gharama yoyote. (3) Waziri, kupitia kanuni, anaweza kuamua mazingira ambayo katazo la uchakataji wa taarifa binafsi lililoelezwa chini ya kifungu hiki halitaweza kuondelewa hata kwa ridhaa ya mhusika wa taarifa. (4) Endapo mhusika wa taarifa ambaye ridhaa yake inaombwa kwa madhumuni ya Sheria hii ni mtoto, mtu asiyekuwa na akili timamu au mtu mwingine yeyote asiye na uwezo wa kutoa ridhaa, ridhaa ya mtu huyo itapatikana kutoka kwa mzazi, mlezi, mrithi, wakili wake au mtu mwingine yeyote anayetambulika kisheria kwa niaba yake anayepaswa kutoa ridhaa. (5) Kifungu kidogo cha (1) hakitatumika iwapo(a) uchakataji ni muhimu kwa uzingatiaji wa sheria nyingine; (b) uchakataji ni muhimu kulinda maslahi muhimu ya mhusika wa taarifa au ya mtu mwingine, iwapo mhusika wa taarifa hawezi kutoa ridhaa yake au hajawakilishwa na mwakilishi wake kisheria; (c) uchakataji ni muhimu kwa ajili ya kufungua, uendeshaji au utetezi wa madai ya kisheria; (d) uchakataji unahusiana na taarifa binafsi zilizowekwa wazi kwa umma na mhusika wa taarifa; (e) uchakataji ni muhimu kwa madhumuni ya tafiti ya kisayansi na Tume, kwa miongozo maalum, imeainisha mazingira ambayo uchakataji huo unaweza kufanyika; au (f) uchakataji ni muhimu kwa madhumuni ya kitabibu kwa maslahi ya mhusika wa taarifa, na taarifa binafsi nyeti zinazohusika, zinachakatwa chini ya usimamizi wa mtaalamu wa afya kwa mujibu wa sheria inayosimamia huduma hizo. SEHEMU YA TANO 17

Seleccionar párrafo de destino3

Conectar a un párrafo
Connect to an entity
Disable highlights
Añadir a la tabla de contenidos