Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 42 “mfumo wa kompyuta” maana yake ni kifaa au mchanganyiko wa vifaa, ikijumuisha mtandao, vifaa vya kuingizia na vya kutolea na vinavyoweza kutumika pamoja na majalada ya nje yenye programu za kompyuta, maelekezo ya kielektroniki, data za kuingizia na kutolea zinazotunza data za hesabu za miongo zilizo na mantiki, utunzaji wa data za hesabu na udhibiti wa utolewaji wa mawasiliano na majukumu mengine; “data kompyuta” maana yake ni uwasilishaji wa maelezo, dhana, taarifa au maelekezo katika namna inayofaa kuchakata katika mfumo wa kompyuta,ikijumuisha programu inayofaa kuuwezesha mfumo wa kompyuta kutelekeza kazi fulani; “chombo cha utunzaji wa data ” maana yake ni kifaa chochote au kitu ambacho kwayo kompyuta au taarifa inaweza kutunzwa au kutengenezwa ama kwa msaada wa kifaa kingine au kitu au la; “kifaa” inajumuisha: (a) programu ya kompyuta, namba tambuzi au mianzi laini; (b) sehemu ya mfumo wa kompyuta kama vile grafiki kadi, kadi ya kutunza kumbukumbu, chipu au kichakataji; (c) kifaa cha kutunzia kumbukumbu za kompyuta; na (d) kifaa cha kuingizia na kutolea taarifa katika kompyuta na mifumo ya kompyuta; “mawasiliano ya kielektroniki” maana yake ni uhamishaji wowote wa alama, ishara au data kompyuta ya aina yoyote ile iliyotumwa yote au sehemu yake kwa njia ya waya, redio, elektromagnetiki, picha ya kielektroniki, picha ya

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières