41 Tafsiri No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 3. Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo“kuingia” kuhusiana na mfumo wa kompyuta, maana yake ni kuingia, kutoa maelekezo, kuwasiliana, kuhifadhi data au kupokea data kutoka katika mfumo wa kompyuta au vinginevyo kutumia nyenzo zozote za mfumo wa kompyuta, mtandao au chombo cha kuhifadhia data; “mtoa njia” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya usambazaji wa data za kielekroniki kwa kusambaza taarifa zilizotolewa na, au kwa mtumiaji wa huduma katika mtandao wa mawasiliano au kutoa fursa ya kuingia kwenye mtandao wa kompyuta; “mhifadhi data ” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya uhifadhi wa data za kielektroniki kwa njia inayojiendesha yenyewe, kwa kupitia mtu kati au kwa utunzaji wa taarifa wa muda mfupi, kwa madhumuni ya kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa kwa watumiaji wengine wa huduma kiufanisi zaidi, pale watakapoomba; “mtoto” maana yake ni mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na nane; “ponografia za watoto” maana yake ni aina ya picha na filamu za ngono zinazoashiria au kumuonesha: (a) mtoto akiwa anashiriki kwa uwazi matendo ya ngono; (b) mtu anayeonekana kama mtoto akiwa anashiriki kwa uwazi matendo ya ngono; au (c) taswira inayoashiria mtoto akiwa anashiriki kwa uwazi matendo ya ngono;

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières