Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 46 (ii) mawasiliano yasiyo ya umma ya kieletromaniginetiki yatokanayo katika mfumo wa kompyuta usio wa umma; au (iii) mfumo wa kompyuta usio wa umma ambao umeunganishwa na mfumo mwingine wa kompyuta; au (b) anakwepa hatua za udhibiti zilizoelekezwa kwa ajili ya kukinga kuingiliwa kwa maudhui yaliyomo kwenye mawasiliano yasiyo ya umma. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. Kuingilia data kinyume cha sheria 7.-(1) Mtu ambaye kwa makusudi na kinyume cha sheria(a) (b) (c) (d) anaharibu au anazorotesha data kompyuta; anafuta data kompyuta; anabadili data kompyuta; anaifanya data kompyuta ipoteze maana, ishindwe kutumika au ikose ufanisi; (e) anazuia au anaingilia matumizi halali ya data kompyuta; (f) anamzuia au anamuingilia mtu mwingine anayetumia data kompyuta kihalali; au (g) anamzuia mtu aliyeidhinishwa kutumia data kompyuta, atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume na sheria au kutumikia, au yoyote iliyokubwa kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières