49 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 mtu yoyote kuingilia mfumo wa kompyuta au sehemu yake kwa lengo la kutenda kosa. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja. Kughushi kunakohusiana na masuala ya kompyuta 1 1 -( 1) Mtu hataingiza, hatabadilisha, hatachelewesha, hatasambaza au hatafuta data kompyuta iliyoghushiwa kwa lengo la kutaka itumike bila kujali kama taarifa hiyo inasomeka au haisomeki. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja. Udanganyifu 12.-(1) Mtu hatasababisha upotevu kwa mali ya mtu unaohusiana na mwingine kwakompyuta (a) kuongeza, kubadilisha, kufuta, kuchelewesha kusambaza au kuzuia data kompyuta; au (b) kuingilia utendaji kazi wa mfumo wa kompyuta, kwa udanganyifu au uongo kwa lengo la kujipatia bila haki manufaa ya kiuchumi.

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières