Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 58 (c) limetendwa na Mtanzania; au (d) limetendwa na Mtanzania anayeishi nje Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, endapo kitendo alichokitenda mtu huyo kingekuwa ni kosa chini ya sheria ya nchi hiyo; (e) limetendwa na mtu yeyote, bila kujali utaifa au ukaazi wake au eneo husika, iwapo kosa limefanyika(i) kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kifaa au data zilizoko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; au (ii) dhidi ya mfumo wa kompyuta, kifaa au data au mtu aliye ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (2) Katika kifungu hiki, neno “mahakama” lina maana ya mahakama yenye mamlaka. SEHEMU YA NNE UPEKUZI NA UKAMATAJI Upekuzi na ukamataji 31.-(1) Askari polisi mkuu wa kituo au afisa utekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa kituo, baada ya kuridhika kuwa kuna sababu za msingi kushuku au kuamini kuwa mfumo wa kompyuta(a) unaweza kutumika kuthibitisha kosa; au (b) unachukuliwa na mtu yeyote kutokana na kosaInaweza kutoa hati ya upekuzi itakayo muidhinisha afisa utekelezaji wa sheria (i) kuingia kwenye eneo kwa lengo la kupekua au kukamata kifaa au mfumo wa kompyuta; (ii) kuiwekea ulinzi data kompyuta iliyopatikana; au

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières