Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 68 (a) (b) (c) (d) majina kamili na anuani; saini ya mlalamikaji; maelezo ya haki inayodaiwa kuvunjwa; maelezo juu ya kitu au shughuli ambayo inadaiwa kuwa chimbuko la kitendo kilicho kinyume na sheria; (e) hatua ya utatuzi inayotakiwa kuchukuliwa na mtoa huduma kuhusiana na lalamiko; (f) maelezo kuwa mlalamikaji anafanya hivyo kwa nia njema; (g) maelezo ya mlalamikaji kuwa, kwa ufahamu wake, taarifa iliyomo kwenye taarifa zilizochukuliwa ni sahihi. (3) Mtu anayewasilisha taarifa kwa mtoa huduma kuhusiana na muamala usio halali, huku akijua kuwa taarifa hiyo ni potofu, atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atatakiwa kulipa faini ya shilingi million tano au kifungo cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. (4) Mtoa huduma atakayeshindwa kuchukua hatua juu ya notisi ya kuondoa aliyoipokea kwa mujibu wa Sheria hii, atashitakiwa kwa kosa la kuainisha taarifa chini kifungu kidog cha ( 1). (5) Mtu anayetoa notisi ya kuondoa kwa mtoa huduma, na mtoa huduma akashindwa kufanyia kazi notisi hiyo, mtu huyo anaweza kutoa taarifa kwa mamlaka husika kwa kushindwa kutekeleza notisi na mamlaka husika inaweza kumchukulia hatua mtoa huduma au kumtaka mtoa huduma huyo kuifanyia kazi notisi hiyo au kuchukua hatua yoyote kulishughulikia suala hilo. (6) Mtoa huduma hatawajibika kwa kuondoa taarifa ikiwa ameifanya kwa mujibu wa Sheria hii. Wajibu mwingine kutoadhiriwa na sheria 46. Sehemu hii haitaathiri wajibu wa mtoa huduma: (a) uliyotolewa kwa makubaliano; (b) ambaye anatenda kwa namna hiyo chini ya leseni

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières