Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 na Rais kwa kuzingatia utaratibu kwamba iwapo Mwenyekiti anatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, Makamu Mwenyekiti atatoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano. (3) Wajumbe wengine watano chini ya kifungu kidogo cha (1)(b) watateuliwa na Waziri kutoka miongoni mwa watu wenye sifa na uzoefu katika eneo la TEHAMA, sheria, uhandisi, fedha au utawala. (4) Ili kudumisha uadilifu wa Tume na kwa madhumuni ya kuepusha mgongano wa maslahi, mtu hatakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume iwapo kutokana na aina ya madaraka aliyonayo anaweza kuwa na ushawishi kwa Tume. (5) Mkurugenzi Mkuu wa Tume atakuwa katibu wa Bodi. (6) Masuala mengine kuhusu Bodi na uendeshaji wa shughuli zake yatakuwa kama ilivyoainishwa katika Jedwali. Majukumu ya Bodi 9.-(1) Bodi itasimamia utendaji wa Tume ili kuhakikisha kuwa utendaji huo unazingatia sheria na taratibu zinazosimamia Tume. (2) Bila kuathiri ujumla wa kifungu kidogo cha (1), Bodi itakuwa na wajibu wa(a) kutoa miongozo ya kimkakati na kuunda sera za uendeshaji na usimamizi wa Tume; (b) kusimamia shughuli na utendaji kazi wa menejimenti ya Tume; (c) kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali, ikijumuisha kuidhinishwa kwa mpango kazi wa mwaka, bajeti ya mwaka na bajeti ya nyongeza; (d) kuidhinisha mipango ya uwekezaji ya Tume; (e) kuidhinisha ripoti za utendaji kazi wa Tume; (f) kuidhinisha kanuni za maadili kwa watumishi wa Tume; (g) kuidhinisha na kusimamia taratibu za usimamizi wa fedha na kanuni za utumishi wa Tume; (h) kuidhinisha uondoshaji wa mali za Tume; na (i) kutekeleza wajibu mwingine wowote kwa kadri 10

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières