Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
uchunguzi
ya Sheria hii, Tume, katika namna itakayoainishwa katika
kanuni, inapaswa kumpa notisi ya uchunguzi mkusanyaji
au mchakataji anayehusika na malalamiko na nia ya
kufanya uchunguzi katika suala hilo.
Usiri wa
uchunguzi
41.-(1) Uchunguzi wa malalamiko chini ya Sheria hii
utafanyika kwa siri.
(2) Mkurugenzi Mkuu au mtu yeyote anayefanya
kazi kwa niaba yake ya kupokea taarifa binafsi zinazohusu
uchunguzi wowote chini ya Sheria hii au sheria nyingine
yoyote, atapaswa kukidhi matakwa yoyote ya kiusalama
kwa kuchukua kiapo cha usiri kinachopaswa kuchukuliwa
na watu ambao wanatekeleza majukumu kama hayo.
Mamlaka ya
Tume wakati
wa uchunguzi
42.-(1) Wakati wa kuchunguza malalamiko, Tume
itakuwa na mamlaka ya(a) kuita na kumtaka mtu kuhudhuria mbele ya
Tume;
(b) kupokea na kukubali ushahidi na taarifa
nyingine, kwa kiapo au kwa hati ya kiapo au
vinginevyo;
(c) kuingia katika jengo lolote linalomilikiwa na
mkusanyaji au mchakataji yeyote kwa ajili ya
kujiridhisha endapo jengo hilo linakidhi
mahitaji ya usalama;
(d) kumhoji mtu yeyote au kuondoka na kifaa
chochote chenye taarifa binafsi katika jengo
lolote alimoingia kwa mujibu wa aya (c); na
(e) kuchunguza au kupata nakala za, au dondoo
kutoka
kwenye
vitabu,
nyaraka
au
kumbukumbu nyingine zilizopatikana katika
jengo alimoingia kwa mujibu wa aya (c) zenye
suala lolote linalohusika na uchunguzi.
(2) Wakati wa uchunguzi wa malalamiko chini ya
kifungu hiki, mlalamikaji na mkusanyaji au mchakataji
anayelalamikiwa anaweza kupewa nafasi ya kufanya
mawasilisho kwa Tume.
24
Sélectionner le paragraphe cible3
Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières