Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA. 11 YA 2022 NAKUBALI, SAMIA SULUHU HASSAN Rais 27 Novemba, 2022 Sheria kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa lengo la kuweka kiwango cha chini cha matakwa ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi, kuanzisha Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi zinazochakatwa na vyombo vya Serikali na vyombo binafsi, na masuala mengine yanayohusiana na hayo. IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI Jina na kuanza kutumika Matumizi Tafsiri 1. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 na itaanza kutumika katika tarehe ambayo Waziri atateua kwa notisi katika Gazeti la Serikali. 2. Sheria hii itatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar isipokuwa kwa Tanzania Zanzibar haitatumika kwa mambo yasiyo ya muungano. 3. Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo“afisa ulinzi wa taarifa binafsi” maana yake ni mtu aliyeteuliwa na mkusanyaji au mchakataji na kupewa jukumu la kuhakikisha utekelezaji wa 4

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières