Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (b) ikiwa imechakatwa, ni taarifa binafsi inayoonyesha asili ya rangi au kabila, itikadi za kisiasa, imani za kidini au kifalsafa, ushirika, uanachama wa vyama vya wafanyakazi, jinsia na taarifa za kiafya au mahusiano ya kingono; na (c) taarifa binafsi yoyote ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi inachukuliwa kuwa ina athari kubwa kwa haki na maslahi ya mhusika wa taarifa; “taarifa za vinasaba” maana yake ni taarifa binafsi yoyote inayotokana na uchambuzi wa tindikali ya vinasaba; “Tume” maana yake ni Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 6; “uchakataji” maana yake ni uchambuzi wa taarifa binafsi, kwa njia za kiotomatiki au vinginevyo, kama vile kukusanya, kurekodi au kushikilia taarifa binafsi au kufanya uchambuzi kwenye taarifa binafsi, ikiwa ni pamoja na(a) kuzipanga upya, kuzichukua na kuzitumia kama zilivyo au kuzibadilisha; (b) kuzirejesha au kuzitumia; au (c) kuziwianisha, kuzichanganya, kuzuia matumizi yake, kuzifuta au kuziharibu; “usafirishaji wa taarifa binafsi kwenda nje ya nchi” maana yake ni usafirishaji wowote wa taarifa binafsi wa kimataifa, unaovuka mipaka kwa njia za kielektroniki au njia nyingine; na “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya masuala ya mawasiliano. Malengo ya Sheria 4. Malengo ya Sheria hii ni(a) kudhibiti ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi; (b) kuhakikisha kwamba ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi za mhusika wa taarifa unaongozwa na misingi iliyowekwa katika Sheria hii; (c) kulinda faragha za watu binafsi; (d) kuweka utaratibu wa kisheria na kitaasisi wa kulinda taarifa binafsi; na 7

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières