Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 Tume itakavyoona inafaa kwa ajili ya kutimiza malengo yake kwa mujibu wa Sheria hii. Kamati za Bodi 10. Bodi inaweza, kwa madhumuni ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kuunda na kuteua kutoka miongoni mwa wajumbe wake, kamati zozote kadri itakavyoona inafaa. Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu 11.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ambaye atateuliwa na Rais. (2) Mtu atateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu ikiwa ana sifa zifuatazo: (a) amehitimu katika chuo kikuu kinachotambulika na ana angalau shahada ya kwanza katika nyanja za TEHAMA, uhandisi, sheria, uchumi, fedha au utawala; (b) ana uzoefu wa utumishi usiopungua miaka kumi katika angalau moja ya nyanja zilizotajwa katika aya (a); na (c) ana ujuzi au utaalamu katika nyanja ya ulinzi wa taarifa. Muda wa kuhudumu wa Mkurugenzi Mkuu 12. Mkurugenzi Mkuu atashika madaraka kwa kipindi cha miaka mitano na baada ya kipindi hicho kumalizika, anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja. Watumishi wa Tume 13.-(1) Tume, kwa kuzingatia sheria za utumishi wa umma, itaajiri watumishi kwa idadi itakayohitajika kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu ya Tume. (2) Tume inaweza kuteua washauri na wataalam katika taaluma mbalimbali kwa kuzingatia vigezo na masharti yatakayowekwa na Tume. SEHEMU YA TATU USAJILI WA WAKUSANYAJI NA WACHAKATAJI WA TAARIFA BINAFSI Usajili wa wakusanyaji na wachakataji 14.-(1) Mtu hatakusanya au kuchakata taarifa binafsi bila kusajiliwa kama mkusanyaji au mchakataji chini ya Sheria hii. (2) Mtu anayekusudia kukusanya au kuchakata 11

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières