Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (3) Bila kujali sheria nyingine yoyote, Tume inaweza kuchunguza taarifa binafsi iliyorekodiwa katika namna yoyote inayohifadhiwa na mkusanyaji au mchakataji, na katika kufanya hivyo, Tume haitazuiliwa kupata taarifa yoyote. (4) Nyaraka au andiko lolote litakalotolewa chini ya kifungu hiki na mkusanyaji au mchakataji au mtu mwingine yeyote, litarejeshwa na Tume ndani ya siku kumi za kazi baada ya maombi kuwasilishwa kwa Tume na mkusanyaji au mchakataji au mtu huyo, lakini hakuna chochote katika kifungu kidogo hiki kitakachoizuia Tume kuhitaji nyaraka au andiko hilo kuwasilishwa tena kwa mujibu wa kifungu hiki. Kuizuia Tume Kutumia msaada wa mtu au mamlaka nyingine 43. Mtu ambaye, kuhusiana na utekelezaji wa mamlaka iliyotolewa chini ya Sheria hii(a) ataizuia au kuikwamisha Tume katika utekelezaji wa mamlaka yake; (b) atashindwa kutoa msaada au taarifa zilizoombwa na Tume; (c) atakataa kuiruhusu Tume, inapotekeleza majukumu yake, kuingia katika majengo yoyote au kuondoka na nyaraka au kifaa chochote chenye taarifa binafsi; au (d) ataipa Tume taarifa yoyote ambayo ni ya uongo au ya kupotosha, anatenda kosa na endapo atatiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja. 44.-(1) Kwa madhumuni ya kukusanya taarifa au kwa uchunguzi wowote chini ya Sheria hii, Tume inaweza kushirikiana au kumtumia mtu au mamlaka nyingine yoyote kama itakavyoona inafaa kwa ajili ya kuisaidia Tume katika utekelezaji wa majukumu yake. (2) Mtu au mamlaka nyingine itakayoshirikishwa au kutumiwa na Tume kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1), itakuwa na mamlaka sawa na mamlaka iliyo nayo Tume katika kutekeleza mamlaka ya uchunguzi kwa mujibu wa Sheria hii. 25

Sélectionner le paragraphe cible3

Se connecter à un paragraphe
Connect to an entity
Disable highlights
Ajouter à la table des matières