Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 taarifa chini ya kifungu kidogo cha (4), Tume itazingatia idadi ya watu ambao watapaswa kuarifiwa. Kurekebisha, kuzuia, kufuta na kuharibu taarifa binafsi 38.-(1) Pale ambapo Tume itaridhika kwa maombi ya mhusika wa taarifa kuwa taarifa binafsi zinazomhusu mhusika huyo siyo sahihi, Tume inaweza kumuamuru mkusanyaji au mchakataji kurekebisha, kuzuia, kufuta au kuharibu taarifa hizo. (2) Kifungu kidogo cha (1) kitatumika hata kama taarifa binafsi ni kumbukumbu sahihi zilizopokelewa na mkusanyaji au mchakataji kutoka kwa mhusika wa taarifa au mtu mwingine. (3) Pale ambapo taarifa binafsi siyo sahihi, Tume inaweza kumuelekeza mkusanyaji au mchakataji kurekebisha taarifa hizo kwa kadri itakavyoona inafaa. (4) Pale ambapo taarifa binafsi zinazolalamikiwa zimerekebishwa, zimezuiwa, zimehuishwa, zimefutwa au zimeharibiwa chini ya kifungu hiki, mkusanyaji au mchakataji atatakiwa kuwataarifu wahusika wengine ambao walipatiwa taarifa binafsi husika kuhusu kurekebishwa, kuzuiwa, kuhuishwa, kufutwa au kuharibiwa kwa taarifa hizo. SEHEMU YA SABA UCHUNGUZI WA MALALAMIKO Malalamiko dhidi ya ukiukwaji wa misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi Notisi ya 39.-(1) Mtu yeyote atakayebaini kuwa mkusanyaji au mchakataji amekiuka misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi anaweza kuwasilisha malalamiko kwa Tume. (2) Pale ambapo Tume imejiridhisha kuwa kuna sababu za msingi za kuchunguza suala chini ya Sheria hii, Tume inaweza kuanzisha uchunguzi wa malalamiko kuhusiana na suala hilo. (3) Malalamiko yatakayowasilishwa katika kifungu hiki yatachunguzwa na kumalizika ndani ya siku tisini tangu tarehe ya kupokelewa. (4) Tume inaweza, kwa kuzingatia mazingira ya malalamiko, kuongeza muda ulioainishwa chini ya kifungu kidogo cha (3) kwa kipindi kisichozidi siku tisini. 40. Kabla ya kuanza uchunguzi wa malalamiko chini 23

Select target paragraph3

Connect to a paragraph
Connect to an entity
Disable highlights
Add to table of contents