Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 70 Makosa yanayofanywa na kampuni hodhi 49. Endapo kampuni inatiwa hatiani kwa kosa chini ya Sheria hii, mtu yeyote ambaye wakati wa utendaji wa kosa(a) alikuwa ni mkurugenzi, afisa au vinginevyo anahusika na mambo ya utawala wa kampuni hodhi hiyo; (b) huku akiwa anajua, aliruhusu kitendo kilichopelekea kosa hilo atachukuliwa kuwa ametenda kosa hilo, isipokuwa kama itathibitishwa wakati kosa hilo linatendeka, lilitendeka bila idhini yake na alifanya jitihada za kutosha kuzuia kutendeka kwa kosa hilo, atachukuliwa kuwa ametenda kosa hilo na anaweza kushitakiwa na kuadhibiwa ipasavyo. Kufifilisha kosa 50.-(1) Bila ya kuathiri sheria nyingine inayotumika Tanzania Bara, Mkurugenzi wa Mashtaka, anaweza, muda wowote kabla ya mwenendo wa mahakama kuanza na kwa kuzingatia tamko la kukiri kosa kwa hiari la mshitakiwa anaweza kufifilisha kosa na kuamuru mtu huyo alipe kiasi cha pesa atakachokitaja ambacho hakitazidi kiasi cha faini kwa kosa lolote hilo. (2) Amri ya kufifilisha kosa chini ya kifungu kidogo cha ( 1) itakuwa (a) ki maandishi, ikiainisha kosa lililotendeka, kiasi cha fedha zitakazolipwa na tarehe ya kufanya malipo ikiambatanisha tamko la kukubali kosa lililorejewa chini ya kifungu kidogo cha ( 1); (b) ni uamuzi wa mwisho na hautakatiwa rufaa; na (c) na uwezo wa kutekelezwa katika namna sawa na amri ya Mahakama Kuu.

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات