53 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 Ujumbe unaotumwa bila ridhaa 20.-(1) Mtu ambaye kwa nia ya kutenda kosa chini ya Sheria hii:(a) hataanzisha usambazaji wa ujumbe unaotumwa bila ridhaa; (b) hatarusha tena au kusambaza upya ujumbe unaotumwa bila ridhaa; (c) hataghushi ujumbe wa utambulisho na kutuma bila ridhaa. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. (3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “taarifa zinazotumwa bila ridhaa” maana yake ni taarifa au data za kielektroniki amabazo hazijaombwa na mpokeaji. Ufichuaji wa taarifa za upelelezi 21.-(1) Mtu kwa makusudi na kunyume na sheria hatatoa, taarifa yoyote inayohusiana na upelelezi wa jinai, inayohitaji usiri. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja. Kuzuia upelelezi 22. Mtu ambaye kwa makusudi na kinyume cha sheria ataharibu, atafuta, ataondoa, ataficha, atabadilisha au ataifanya data kompyuta kukosa maana, kutofanya kazi au kutotumika kwa lengo la kuharibu ushahidi au kuchelewesha upelelezi atakuwa

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات