Na.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 54 ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua milioni tatu au kutumikia kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. (2) Mtu ambaye kwa makusudi atazuia utekelezaji au atashindwa kutekeleza amri iliyotolewa na sheria hii, atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja. Unyanyasaji kwa kupitia mtandao 23.-(1) Mtu hataanzisha au kukadimisha mawasiliano yoyote ya kielektroniki kwenda kwa mtu yoyote kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kwa lengo la, kulazimisha, kutisha au kunyanyasa au kusababisha maudhi ya hisia. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja. Ukiukaji wa haki bunifu 24.-(1) Mtu hatatumia mfumo wa kompyuta kwa lengo la kukiuka haki bunifu zinazolindwa na sheria nyingine yoyote. (2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika iwapo ukiukaji (a) hauhusiani na masuala ya kibiashara, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja; (b) unagusa masuala ya kibiashara, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات