67 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 (b) baada ya kufahamu kuwa taarifa zilizo kinyume na sheria zilizotunzwa kwa njia nyingine zaidi ya amri ya mamlaka ya umma, haraka iwezekanavyo anaitaarifu mamlaka husika. Mtoa huduma ya utafutaji wa taarifa 44.-(1) Mtoa huduma ya utafutaji wa taarifa hatawajibika kwa matokeo ya utafutaji huo, kwa masharti kwamba(a) haanzishi mawasiliano; (b) hachagui mpokeaji wa mwasiliano; na (c) hachagui au kubadilisha taarifa iliyoko kwenye mawasiliano. (2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “mtoa huduma ya utafutaji wa taarifa” maana yake ni mtu anayetengeneza au anayeendesha huduma ambayo inatafuta taarifa inayotengeneza kiashiria cha taarifa za mtandao au anawezesha upatikanaji wa vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya utafutaji wa taarifa inayotolewa na mtu wa tatu. Notisi ya kuondoa 45. -(1) Mtu anaweza, kupitia notisi ya kuondoa, kumtaarifu mtoa huduma kuhusu(a) data au taarifa iliyomnyima mpokeaji au mtu wa tatu haki ya huduma; (b) vitu au shughuli yoyote ambayo ni kinyume cha sheria; au (c) suala lolote linalotekelezwa au linalotolewa kinyume cha Sheria hii au sheria nyingine. (2) Kwa madhumuni ya Sehemu hii, notisi ya kuondoa itakuwa katika hali ya kudumu ikitumwa na mlalamikaji kwenda kwa mtoa huduma au wakala wake, na itajumuisha-

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات