69 No.14 Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 au mfumo mwingine wa usimamizi uliotajwa chini ya sheria yoyote; (c) uliyotolewa na sheria au amri ya mahakama ili kutoa, kuzuia au kukataza uingiaji kwenye mawasiliano ya kieletroniki au kusitisha au kuzuia kitendo kisicho cha halali. SEHEMU YA SITA MASHARTI YA JUMLA Kinga 47. -(1) Bila ya kujali sheria nyingine yoyote kinyume na haya, jambo au kitu chochote kitakachofanywa na afisa utekelezaji wa sheria, katika utekelezaji wa majukumu yake chini ya Sheria hii, hakitasababisha afisa utekelezaji wa sheria kuwajibika binafsi kwa jambo au kitu hicho. (2) Mtu hatawajibika kuhusiana na utekelezaji wa kitendo chochote au kutokutenda, iwapo kitendo hicho au kutokutenda huko kulifanywa kwa nia njema na si kwa uzembe kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii. Utaifishaji mali 48. -(1) Pamoja na adhabu iliyotolewa chini ya Sheria hii, mahakama inaweza kutoa amri kwa ajili ya utaifishaji wa(a) mali yoyote inayoonekana kuwa ni sehemu ya mapato yatokanayo na kosa; na (b) chombo au mali yoyote iliyotumika au inayokusudiwa kutumika kutenda au kufanikisha utendaji wa kosa. (2) Pamoja na amri iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha ( 1), mahakama inaweza kumuamuru mtu aliyetiwa hatiani kumlipa fidia mtu aliyeathirika na kosa hilo kwa kadri ambavyo mahakama itaona inafaa.

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات