Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 sheria zake, ikiwa mkusanyaji ataihakikishia Tume kwamba kuna ulinzi wa kutosha wa taarifa binafsi, uhuru na haki za msingi za mhusika wa taarifa, na utekelezaji wa haki za mhusika wa taarifa, na kwamba ulinzi huo unaweza kutekelezwa kupitia hatua zinazojitosheleza za kisheria, kiusalama na masharti husika ya mkataba. SEHEMU YA SITA HAKI ZA WAHUSIKA WA TAARIFA Haki ya kupata taarifa binafsi 33.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, mhusika wa taarifa ana haki ya(a) kufahamishwa na mkusanyaji yeyote endapo taarifa binafsi zinachakatwa na mkusanyaji huyo au mkusanyaji mwingine kwa niaba ya mkusanyaji huyo; (b) kupewa na mkusanyaji maelezo ya(i) taarifa binafsi zinazomhusu; (ii) madhumuni ya uchakataji; na (iii) wapokeaji au makundi ya wapokeaji waliopewa au wanaoweza kupewa taarifa hizo; (c) pale ambapo uchakataji wa taarifa binafsi kwa njia ya kiotomatiki kwa madhumuni ya kutathmini masuala yanayomhusu, umetumika au unaweza kutumika kama msingi pekee wa maamuzi yenye athari kubwa kwake, kufahamishwa na mkusanyaji kuhusu sababu zilizotumika kufikia uamuzi huo. (2) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo cha (1), mkusanyaji hatalazimika kutoa taarifa kwa mhusika wa taarifa endapo taarifa hizo(a) siyo sahihi; (b) zinahusika katika uchunguzi kwa mujibu wa sheria; au (c) zimezuiliwa kwa amri ya mahakama. Haki ya kuzuia uchakataji unaoweza kumuathiri mhusika wa taarifa 34.-(1) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (2), mhusika wa taarifa ana haki ya kumtaka mkusanyaji kupitia utaratibu utakaoainishwa katika kanuni, kusitisha au kutoanza uchakataji wa taarifa binafsi yoyote 20

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات