Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 itakuwa na uwezo wa(a) kumiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika, kutoa mali na kuingia mikataba au makubaliano mengine yoyote; (b) kushtaki au kushtakiwa; na (c) kutekeleza jukumu lolote lingine ambalo taasisi nafsi yoyote kisheria inaweza kutekeleza kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake chini ya Sheria hii. Majukumu ya Tume Uanzishwaji wa Bodi 7. Majukumu ya Tume yatakuwa(a) kufuatilia utekelezaji wa Sheria hii kwa wakusanyaji na wachakataji; (b) kusajili wakusanyaji na wachakataji kwa mujibu wa Sheria hii; (c) kupokea, kuchunguza na kushughulikia malalamiko kuhusu madai ya ukiukwaji wa ulinzi wa taarifa binafsi na faragha za watu; (d) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya jambo lolote ambalo Tume itaona linaathiri ulinzi wa taarifa binafsi na faragha za watu; (e) kutoa elimu kwa umma kwa kadri itakavyofaa kwa madhumuni ya utekelezaji wa Sheria hii; (f) kufanya tafiti na kufuatilia maendeleo ya teknolojia kuhusiana na uchakataji wa taarifa; (g) kuanzisha utaratibu wa ushirikiano na mamlaka za nchi nyingine zinazosimamia ulinzi wa taarifa binafsi na kuishauri Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa Sheria hii; na (h) kutekeleza majukumu mengine ya Tume kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya Sheria hii. 8.-(1) Inaanzishwa Bodi itakayojulikana kama Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo itakuwa ni chombo cha usimamizi wa Tume na ambayo itakuwa na wajumbe saba kama ifuatavyo: (a) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti; na (b) wajumbe wengine watano. (2) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watateuliwa 9

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات