Na 11 Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 taarifa atawasilisha maombi ya usajili kwa Tume. (3) Tume inaweza, katika muda utakaoainishwa katika kanuni, kukubali au kukataa maombi yaliyowasilishwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2). (4) Tume itatoa cheti cha usajili kwa mkusanyaji au mchakataji aliyekidhi matakwa ya usajili na kusajiliwa chini ya kifungu hiki. (5) Endapo Tume itakataa maombi ya usajili itapaswa kumtaarifu mwombaji kwa maandishi juu ya uamuzi wake na sababu ya uamuzi huo. Rejesta ya wakusanyaji na wachakataji 15.-(1) Tume itaanzisha na kutunza rejesta ya wakusanyaji na wachakataji waliosajiliwa kwa mujibu wa Sheria hii. (2) Rejesta ya wakusanyaji na wachakataji itajumuisha taarifa kama itakavyoainishwa katika kanuni. (3) Mkusanyaji au mchakataji anaweza, wakati wowote, kuomba kwa Tume kuhuisha au kubadili taarifa yoyote iliyoingizwa katika rejesta. Kipindi cha usajili 16.-(1) Kipindi cha usajili kitakuwa ni miaka mitano kuanzia tarehe ya kutolewa kwa cheti cha usajili. (2) Maombi ya kuhuisha usajili yatawasilishwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu kabla ya tarehe ya kuisha kwa kipindi cha usajili kama itakavyoainishwa katika kanuni. Ukaguzi wa taarifa zilizosajiliwa 17. Kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa kwenye kanuni na baada ya kulipwa kwa ada iliyoainishwa, Tume inaweza kuruhusu mtu yeyote kupekua na kupakua taarifa yoyote iliyoingizwa katika rejesta. Kufutwa kwa usajili 18. Tume inaweza kufuta usajili uliofanyika chini ya Sheria hii kwa utaratibu utakaoainishwa katika kanuni. Makosa yanayohusiana na usajili 19. Mtu atakayekiuka masharti ya Sehemu hii au kutoa taarifa za uongo au za kupotosha wakati wa usajili au uhuishaji anatenda kosa na endapo atatiwa hatiani atawajibika kwa adhabu iliyoainishwa katika kifungu cha 63. 20. Mtu yeyote ambaye hataridhika na uamuzi wa Rufaa kuhusiana na 12

اختر الفقرة المستهدفة3

الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات