Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
(a) anatambua madhumuni ya ukusanyaji wa
taarifa binafsi;
(b) anafahamu kuwa ukusanyaji wa taarifa binafsi
ni kwa madhumuni yaliyoidhinishwa; na
(c) anawafahamu wapokeaji wa taarifa binafsi
waliokusudiwa.
(3) Mkusanyaji hatalazimika kuzingatia kifungu
kidogo cha (1) iwapo(a) taarifa binafsi husika zimekwisha wekwa wazi;
(b) mhusika wa taarifa binafsi ameidhinisha taarifa
zake kukusanywa kutoka kwa mtu mwingine;
(c) utekelezaji wake umeshindikana katika
mazingira husika;
(d) kutokutekelezwa kwake ni kwa mujibu wa
sheria; na
(e) utekelezaji wake unaweza kuathiri madhumuni
ya ukusanyaji.
Usahihi wa
taarifa binafsi
24. Kwa kuzingatia madhumuni ambayo taarifa binafsi
zinapendekezwa kutumika, mkusanyaji ambaye ana taarifa
binafsi hatatumia taarifa hizo kwa mazingira yaliyopo bila
kuchukua hatua zinazohakikisha kuwa taarifa hizo
zimekamilika, ziko sahihi, zinaendana na maudhui na
hazipotoshi.
Taarifa binafsi
kutumika kwa
madhumuni
yaliyokusudiwa
25.-(1) Taarifa binafsi zilizokusanywa kwa mujibu wa
Sheria hii zitatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
(2) Endapo mkusanyaji ana taarifa binafsi ambazo
amekusanya kwa madhumuni maalum, anaweza kutumia
taarifa hizo kwa madhumuni mengine iwapo(a) mhusika ameidhinisha matumizi ya taarifa
binafsi kwa dhumuni hilo;
(b) matumizi ya taarifa binafsi kwa dhumuni hilo
yameidhinishwa au kuhitajika kisheria;
(c) dhumuni ambalo taarifa binafsi imetumika
linahusiana moja kwa moja na dhumuni la
ukusanyaji wa taarifa hiyo;
(d) taarifa binafsi inatumika(i) kwa namna ambayo mhusika hatambuliki;
au
(ii) kwa madhumuni ya takwimu au utafiti na
14
اختر الفقرة المستهدفة3
الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات