Na 11
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,
2022
USAFIRISHAJI WA TAARIFA BINAFSI NJE YA NCHI
Kusafirisha
taarifa binafsi
kwenda nchi
yenye ulinzi wa
kutosha wa
taarifa binafsi
31.-(1) Tume inaweza, kwa kuzingatia masharti ya
Sheria hii, kuzuia usafirishaji wa taarifa binafsi kwenda nje
ya nchi.
(2) Taarifa binafsi itasafirishwa kwenda nchi yenye
mfumo wa kisheria unaotoa ulinzi wa kutosha wa taarifa
binafsi pale ambapo(a) mpokeaji atabainisha kuwa taarifa binafsi ni
muhimu kwa utekelezaji wa jukumu lenye
maslahi ya umma au kwa mujibu wa shughuli
halali za mkusanyaji wa taarifa binafsi; au
(b) mpokeaji atabainisha umuhimu wa kusafirisha
taarifa na hakuna sababu ya kudhani kwamba
maslahi halali ya mhusika wa taarifa yanaweza
kuathiriwa na usafirishaji au uchakataji katika
nchi inayopokea.
(3) Mkusanyaji atapaswa, bila kujali kifungu
kidogo cha (2), kufanya tathmini ya awali ya umuhimu wa
usafirishaji wa taarifa binafsi.
(4) Mpokeaji atahakikisha kuwa umuhimu wa
usafirishaji wa taarifa binafsi unaweza kuthibitishwa
baadaye.
(5) Mkusanyaji atahakikisha kwamba mpokeaji
anachakata taarifa binafsi kwa madhumuni ambayo
yalipelekea kusafirishwa kwa taarifa husika pekee.
Kusafirisha
kwenda nchi
isiyo na ulinzi
wa kutosha wa
taarifa binafsi
32.-(1) Taarifa binafsi zitasafirishwa kwenda nchi
nyingine tofauti na zile zilizotajwa katika kifungu cha 31,
ikiwa ulinzi wa kutosha umehakikishwa katika nchi ya
mpokeaji na taarifa inasafirishwa kwa dhumuni la
kuruhusu uchakataji ulioruhusiwa kufanyika na
mkusanyaji.
(2) Utoshelevu wa kiwango cha ulinzi unaotolewa
na nchi nyingine utatathminiwa kwa kuzingatia(a) mazingira yote yanayozunguka usafirishaji wa
taarifa binafsi husika;
(b) aina ya taarifa binafsi;
(c) madhumuni
na
muda
wa
uchakataji
unaopendekezwa;
18
اختر الفقرة المستهدفة3
الاتصال بفقرة
Connect to an entity
Disable highlights
أضف إلى جدول المحتويات